Thursday, December 5, 2013
Friday, November 22, 2013
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), linapenda kukanusha taarifa
zilizoandikwa kwenye Gazeti la ‘The Citizen’ la tarehe 20 Novemba 2013 toleo
Nambari 2980 lililochapishwa kwenye ukurasa wa 15 kwa kichwa cha habari ‘From genocide suspects to a DRC rebel faction – 2’
Katika taarifa hiyo, mwandishi ametoa tuhuma za
uongo dhidi ya Maafisa wa JWTZ alizozinukuu
kutoka ripoti ya wataalam wa Umoja wa Mataifa( UN Group of Experts Report). Kwa
mujibu wa tuhuma hizo, imeelezwa eti kuwa baadhi ya makanda wa JWTZ wanakisaidia kikundi cha FDLR.
Tuhuma hizo ziliwahi kukanushwa kuwa hazikuwa za ukweli.
JWTZ
linarudia kukanusha tuhuma hiyo na kusisitiza kwamba hakuna Afisa wake yeyote aliyepo kwenye Utumishi ambaye
amejihusisha au kuwa na ushirikiano na kikundi cha FDLR. Pia, hakuna ushahidi wowote
wa kuonesha kuwa Maafisa wa JWTZ waliostaafu ama wamewahi kushirikiana au
wanaendelea kushirikiana na kikundi hiki.
Aidha, hakuna Makamanda wa JWTZ waliopo kwenye Jeshi la Umoja wa
Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO-FIB) ambao wamejihusisha kufanya mazungumzo au kushirikiana
na kupanga mpango wowote na kikundi cha FDLR.
Tuhuma hizo zilizotolewa na mwandishi huyo ni za
uongo na zinalenga kuchafua sifa na rekodi nzuri ya JWTZ na Tanzania kwa ujumla.
Kama inavyofahamika Tanzania imepeleka kikosi
chake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kama sehemu ya FIB chini ya MONUSCO.
Jukumu la FIB ni kusaidia kurejesha Amani eneo la Mashariki, nchini DRC na
hivyo kukabiliana na vikundi mbalimbali vyenye silaha vinavyotishia amani na
usalama katika eneo hilo. FDLR ni sehemu ya vikundi hivyo.
Hivyo inashangaza sana kuona kuwa pamoja na jukumu
hilo muhimu linalofanywa na kikosi cha Tanzania bado tuhuma hizo zinatolewa na
mwandishi huyo.
JWTZ litaendelea kutekeleza wajibu wake ipasavyo
nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa
nidhamu ya hali ya juu, weledi na uadilifu kama ilivyo kawaida yake na kwa
mujibu wa Azimio lililotolewa na Umoja wa Mataifa na pia kwa mujibu wa maamuzi,
malengo na matarajio ya Kanda ya Maziwa Makuu, SADC na AU.
Imetolewa
na Kurugenzi ya
Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es
Salaam, Tanzania.
Thursday, November 21, 2013
Wednesday, November 20, 2013
Tuesday, November 19, 2013
Monday, November 18, 2013
DAWASCO NA OPERESHENI KATA MAJI JIJINI DAR
SHIRIKA LA MAJISAFI NA MAJITAKA DAR ES SALAAM (DAWASCO) LINAHIMIZA WATEJA WAKE
WOTE KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM, MIJI YA KIBAHA NA BAGAMOYO KULIPA BILI ZAO KWA
WAKATI NA KABLA MWEZI HAUJAISHA.
MTEJA ULIYETUMIA HUDUMA YA MAJISAFI NA MAJITAKA, NENDA SASA KALIPIE KABLA HUDUMA
HIYO HAIJASITISHWA NA WAKAGUZI WANAOPITA NYUMBA KWA NYUMBA.
ZOEZI LA USITISHWAJI WA HUDUMA YA MAJI LIMEANZA RASMI NA LITAHUSISHA WAKAZI WOTE
WANAOHUDUMIWA NA DAWASCO.
KUMBUKA PINDI UTAKAPOSITISHIWA HUDUMA HII GHARAMA YA KURUDISHIWA NI TSH 15,000/
= KWA WATUMIAJI WA MAJUMBANI NA TSH 50,000/= KWA TAASISI NA MAKAMPUNI. EPUKA
USUMBUFU LIPIA HUDUMA HII SASA.
MALIPO YAFANYIKE KUPITIA:
LIPA BILI YA MAJI KUPITIA BENKI ZA CRDB- 01J1021921900, NMB-20103300047, BARCLAYS-
0014003711 NA BOA-02022460009; MPESA, TIGOPESA, AIRTEL MONEY NA EZYPESA; MAXMALIPO
NA SELCOM; AKIBA MOBILE, EXIM MOBILE, NMB MOBILE NA TPB POPOTE; ATM ZA UMOJA
SWITCH.
LIPA BILI YAKO YA MAJI UKIWA MAHALI POPOTE NA KWA WAKATI WOWOTE
DAWASCO IMESOGEZA HUDUMA KARIBU NA MTEJA
IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO MAKAO MAKUU
Subscribe to:
Posts (Atom)