THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone:
255-22-2114512, 2116898
Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE
HOUSE,
P.O.
BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA UMMA
Uingereza
inajivunia kuwa nchi inayoongoza katika uwekezaji nchini Tanzania na itaendelea
kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kiuchumi na kuleta maendeleo .
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amemuambia Rais Kikwete wakati wa
mazungumzo yaliyofanyika 10 Downing Street, Leo tarehe 31 March, 14,
ambapo ndipo yalipo Makao Makuu ya Waziri Mkuu wa Uingereza.
"Tunafurahia sana uhusiano wetu na
kujivunia kuwa tunaongoza katika
Uwekezaji nchini Tanzania" Bw. Cameron amesema na kumhakikishia
Rais Kikwete kuwa Uingereza iko tayari kutoa misaada zaidi.
Rais Kikwete amewasili nchini Uingereza tarehe 30 Machi, 2014 kwa ajili ya
ziara ya kikazi ya siku 3 kufuatia mualiko wa Bw. Cameroon ambaye pia amemuomba
Rais Kikwete aendelee kutoa mchango wake wa mawazo katika masuala ya kimataifa
hasa baada ya mwisho wa muda wa malengo ya millennium ya 2015.
"Tunakaribia mwisho wa muda wa malengo ya millennia Mwaka 2015,
tutahitaji kuweka vipaumbele vingine baada ya hivyo kama kuondosha umaskini,
Maji safi na salama, masuala ya ufisadi na utawala bora, natumaini utaendelea
kutoa mchango wako baada ya malengo hayo kufikia tamati" Waziri
Mkuu Cameron amemuambia Rais Kikwete ambapo Rais amekubali ombi hilo na kuahidi
ushirikiano wake.
Mapema leo asubuhi Rais amekutana na mtoto wa Mfalme Prince Andrew katika
makazi ya Malkia ya Buckingham ambapo wamebadilishana mawazo kuhusu mambo
mbalimbali ya Kimataifa na Kijamii.
Kabla ya kwenda Buckingham Rais amefungua mkutano kuhusu uwekezaji na kuelezea
fursa na nafasi zilizopo za uwekezaji nchini Tanzania na kuelezea kwanini
wawekezaji watakuwa wanafanya uamuzi bora kwa kuwekeza Tanzania kuwa ni pamoja
na;
"Fursa nyingi, amani, usalama, soko la kutosha na kubwa kwa vile Tanzania
iko katika Umoja wa Afrika Mashariki, Ukanda wa Maziwa Makuu na Jumuiya ya
Maendeleo ya Kusini mwa Afrika,hivyo kuwa na uhakika wa soko kubwa na
pana" amesema.
Katika ziara yake Rais pia amekutana na Mstahiki Meya wa Jiji la London
Mama Alderman Fiona Woolf na kukaribishwa rasmi Jijini London. Mstahiki
Meya anatarajia kutembelea Tanzania, Mwezi Septemba Mwaka huu.
Rais alipowasili London tarehe 30 Machi,2014, alikutana na Watanzania wanaoishi
nchini Uingereza na kuwaeleza maendeleo yaliyopo nchini Tanzania.
Rais anaendelea na ziara yake nchini Uingereza
Mwisho.
Imetolewa na;
Premi
Kibanga.
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
London Uingereza
31 Machi, 14